Wednesday, November 9, 2016

NUH MZIWANDA KUFUNGA NDOA NA NAWAR IJUMAA HII

Zimewafikia Shilawadu hizi za kumuhusu msanii wa Bongo Fleva hitmaker wa Jikeshupa Nuh Mziwandakuhusu kufunga ndoa na mpenzi wake Nawar ijumaa hii.

Soudy Brown alipenyezewa taarifa na snitch mzuri mzuri kutoka pande za Msasani ambaye alimuona Nuh Mziwanda akipiga story na Baba Mkwe wake, yaani baba mzazi wa Nawar na kugundua kuwa kumbe kilichokuwa kikizungumziwa pale ni mipango ya harusi na inasemekana kuwa ni mahari ya Tsh. Million 2 ndizo ambazo ametakiwa kutoa mkali huyo ili kuchukua jiko.
Amelithibitisha hilo yeye mwenyewe muhusika mkuu Nuh Mziwanda na kuamua kuwakaribisha wote ambao watajisikia kufika. Ni baada ya kupigiwa simu na Soudy Brown na kuulizwa juu ya suala hilo.

No comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments system