MTV Europe music Awards 2016 ilifanyika weekend iliyopita ambapo Mtanzania mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba alikua akiwania tuzo ya BEST AFRICAN ACTambayo ilitangazwa siku ya tukio mshindi ni Mnigeria Wizkid.
https://1fmtz.blogspot.com
Pamoja na kwamba Wizkid alitangazwa mshindi, mtandaoni ilikua inaonyesha Alikibandio anaongoza kwa kupigiwa kura na hapo watu wakaanza kuuliza kwa nguvu imekuaje? hata hivyo kulionekana mabadiliko baadae kwa rekodi hizo kutoonekana mtandaoni baada ya muda kupita.
Taarifa za uhakika kutoka kwenye Management ya Alikiba Exclusive ni kwamba wametumiwa taarifa na MTV EMA kwamba kuna kosa lilitokea lakini wamerekebisha na kumfikishia taarifa Wizkid kwamba tuzo haikuwa yake hivyo itachukuliwa na kupewa Alikiba.
No comments:
Post a Comment