Jinsi smart ni ofisi yako? Nyumba yako jengo? uwanja wa ndege wa eneo lako?
Kama huna uhakika, wewe si peke yake. utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Honeywell kukuta kwamba hata jengo mameneja na wamiliki hawana picha ya wazi ya jinsi smart vituo vyao ni.
Thursday, November 24, 2016
Mtazamo Vs. Ukweli: Ukweli Kuhusu Smart Majengo
Wednesday, November 23, 2016
KILIO KIKUBWA CHAIBUKA DAR MVUA YATIKISA JIJI LEO Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) yatoa tamnko

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) yataadharisha kuhusu uwezekano wa kuja kwa mvua kubwa yenye upepo, yawataka wananchi wachukue tahadhari.
Yasema mabadiliko ya hali ya hewa kwa sasa yanatokana na kuwepo kwa msimu unaotawaliwa na uwepo wa LANINA ambayo ni ongezeko la hali ya baridi katika eneo la Ikweta ya Bahari ya Pasifiki.
Bado matarajio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa na upepo vitaendelea kuwepo katika msimu huu mpaka mwezi Disemba na mabadiliko kidogo yatajitokeza kwa baadhi ya mikoa ambapo mvua zitanyesha kwa wastani.


Diamond na Ommy Dimpoz wazichapa leo.
Siku zimepita na miaka imekwenda hakuna kolabo tuliyoiona lakini “ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni,” ndio tuliyoyaona. Ndipo nikaukumbuka wimbo malkia wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jaydee ‘Siku Hazigandi’ baada ya kuona urafiki uliogeuka undugu wa damu ukiteketea na kugeuka majivu baada ya kuunguzwa na mwanga wa tochi – ni kitu cha kushangaza na kisichowezekana lakini kwa hapo kiliwezekana.
Nilifurahi sana kuna busara iliyotumika kwa kila mmoja kukaa kimya bila ya kumshtumu mwenzake kwa lolote na kila mmoja akifanya kazi kivyake lakini ghafla nuru ya mwanga uliopo kugeuka giza baada ya usiku wa Jumanne hii mtandao wa Instagram ukigeuka uwanja wa ‘Kitchen Party’ kwa Ommy na Diamond kutupiana vijembe vya maneno ya kashfa na kuanza kutoleana siri ambazo kwa mashabiki hatuna uhakika nazo labda wao wenyewe wanajua juu ya ukweli wausemao kwa jamii.
Diamond alianza kwa kuandika kwenye kipande cha video ya wimbo mpya wa Rich Mavoko aliyoiweka kwenye mtandao huo, “Kushindana na Wasio Jua Raha sana hahahahahaha 


…….”
Ommy Dimpoz alijibu kwa kuandika:
Wazee Wa Kupanik Mbona Kama Povuuu Linawatoka #TeamMzikiMzuri VS #TeamUjanjaUjanja
#Kajiandae
#KabaliYao
#WeDontBuyViews
#MeNilijuaTunafanyaMzikiKumbeVitaaa
#NawajuaWazeeWaKuchambaNataniaTu
#PiaNawajuaKwaMitusiLakiniNishajiandaa
#NawaachiaUwanjaMweupeeeWalaSiblokuMtu
#NachangamshaBarazaKidogoooo
#Kajiandae
#KabaliYao
#WeDontBuyViews
#MeNilijuaTunafanyaMzikiKumbeVitaaa
#NawajuaWazeeWaKuchambaNataniaTu
#PiaNawajuaKwaMitusiLakiniNishajiandaa
#NawaachiaUwanjaMweupeeeWalaSiblokuMtu
#NachangamshaBarazaKidogoooo
Diamond alishindwa kuvumilia naye aliandika, “Mtoto wa Kiume kumchukia Mwanaume Mwenzio kisa Kakataa kukupumulia nayo ni #KOKORO.”
Kwa watu wanaofahamu zaidi maneno ya mitaani wanaweza kufahamu kilichoandikwa ndani kina maana gani tena hayapaswi kuandikwa na wasanii wakubwa kama hawa kwenye hadhira hii. Wakati huo huo siku hizi mitandao ya kijamii inatembelewa mpaka na watoto wadogo, je watoto wao au hata ndugu zao wadogo wanaowalea na kuwategemea wakiona mtu anayemuheshimu nyumbani amefanya hivyo mitandaoni unafikiri itakuwaje?
Kumbukeni mlipotoka kwa kuwa ‘Adui yako wa leo ndio rafiki yako wa kesho, na rafiki yako wa leo ndio adui yako wa kesho’.
Basata watoa Tamko nzito kuhusu video mpya ya Rich Mavoko na Diamond Platnumz

Rich Mavoko na Diamond Platnumz wamezichezea sharubu za simba mkali aliyekuwa usingizini.
Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA limehisi kuna udhalilishwaji wa wanawake kwenye video hiyo na limesema litatoa tamko lake iwapo litaifungia video hiyo au lah!
“Ktk kusimamia maadili ktk Sanaa & udhalilishaji wanawake tuko thabiti.Video ya #kokoro ya #Mavoko inapitia uhakiki.Taarifa itatoka,” limeandika baraza hilo kwenye akaunti yake ya Twitter.
Video ya wimbo huo iliyofanyika nchini Afrika Kusini inaonesha wanawake waliopo kwenye Jacuzzi huku maziwa yao yakiwa wazi licha ya kupakwa rangi ya dhahabu.
Tuesday, November 22, 2016
MUSIC: RICH MAVOKO FT DIAMOND PLATNUMZ – KOKORO (LISTEN & DOWNLOAD)
Sunday, November 20, 2016
Wasafi kumleta Amber Rose Dar mwezi ujao December 24
Katika kusherehekea Christmas mwaka huu, WCB wanatarajia kufanya show yao ya kwanza wakiwa pamoja, December 24 iliyopewa jina Wasafi Beach Party jijini Dar es Salaam.
Wasanii wote
wa label hiyo wakiongozwa na Diamond watatumbuiza. Lakini huenda kukawa na ugeni mkubwa wa staa wa nje na tayari meneja wa Diamond, Sallam ametease jina.
Picha: Zari ajiandaa na ujio wa mtoto wa pili na Diamond
Siku zinayoyoma na mwezi ujao panapo majaliwa, Zari atajifungua mtoto wake wa pili na Diamond. Huyo atakuwa mtoto wake wa tano kwa ujumla.
Subscribe to:
Posts (Atom)

