Tuesday, November 8, 2016

1FMTZ: Ruby afunguka juu ya tetesi za kusaini WCB

14727398_334978763549845_6887458174895390720_nMuimbaji wa kike mwenye sauti ya dhahabu kwenye Bongo Fleva, Ruby amefunguka juu ya tetesi zilizosambaa kuwa amesaini kujiunga na lebo ya WCB.
Ruby amepinga kujiunga na lebo hiyo lakini amedai kuwa anapenda kuwa karibu na Diamond kwa ajili ya kujifunza vitu vingi kutoka kwake.

“WCB hawana roho mbaya unaenda tu muda wowote kama unajua ni nini kimekupeleka pale, kwani mimi kuonekana WCB ndio nipo WCB? Diamond ni msanii mwenzangu, nikiwa naye najifunza vitu vingi, it doesn’t mean nikiwa naye nimejiunga WCB. Kumbuka pale kuna studio na kuna producer Lizer pale watu tunataka kufanya naye kazi,” amemuambia mtangazaji wa kipindi cha The Playlist cha Times FM, Lil Ommy.

No comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments system