Tuesday, November 8, 2016

1FMTZ: MALI ZA RICK ROSS ZINAWEZA KUTAIFISHWA KAMA ASIPOKAMILISHA HAYA



Shirika la Kiserikali linalowajibika kukusanya kodi na utekelezaji wa sheria za kodi nchini Marekani ” Internal Revenue Service (IRS)” laanza kumwinda rapper Rick Ross.
Kupitia ripoti ambayo imetolewa na mtandao wa TMZ inasema kwamba Internal Revenue Serviceimemchunguza Ross takribani miaka mitatu na kusema kwamba anadaiwa dola milioni $5.7 za kodi ambazo hakulipa tangu mwaka 2012 hadi 2014, Bad Newz ni kwamba kama akishindwa kulipa kiasi hicho basi Internal Revenue Service inaweza kutaifisha mali zake.
Ishu hiyo siyo kwamba ndio ya kwanza kutokea kwa rapper huyo, mwanadada Iggy Azalea alishawahi kukumbwa na mkasa huo akidaiwa takribani dola $391,000.

No comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments system